Matumizi sahihi ya nyakati husaidia kuelezea Vitendo,matukio, hisia na ukweli halisi wa mambo mbalimbali katika lugha
Nyakati hizi huweza kuwa katika makundi yafuatayo:
-Wakati uliopita
-Wakati uliopo
-Wakati ujao
Nyakati hutusaidia kuelezea vitendo vya watu au viumbe.
Kitendo kinaweza kufanywa na mtu mmoja ( umoja) au wawili( wingi)
Umoja au wingi umegawanywa katika nafsi ya kwaza, ya pili, na ya tatu
Kumbuka: -Mtu anayeongea ni nafsi ya kwanza
-Mtu anayeambiwa ni nafsi ya pili
-Mtu anayezungumziwa akiwa mbali ni nafsi ya tatu
-Wanyama na vitu vinginevyo ni nafsi ya tatu
Kila nafsi ina umoja (singular) na wingi
Nafsi ya kwanza (umoja): Vitendo vinavyohusu msemaji wa sentensi (mimi). Vitendo hivi huambatana na viwakilishi hivi: n-, mimi, -angu,…
Nafsi ya kwanza (wingi): Vitendo vinavyonihusu mimi msemaji na
wenzangu (sisi)- Vitendo hivi hutumia viwakilishi hivi: tu, sisi, -etu,…
Nafsi ya pili (umoja): Vitendo vinavyohusu mtu anayeambiwa(wewe). Vitendo hivi huambatana na viwakilishi: u- wewe, -ako
Nafsi ya pili ( wingi): Vitendo vinavyohusu watu wengi
wanaosikiliza (nyinyi). Vitendo hivi huambatana na viwakiliishi hivi: m-, nyinyi, -enu…
Nafsi ya tatu ( umoja): Huhusu mtu anayezungumziwa (yeye).
Nafsi ya tatu ( wingi): Vitendo vinavyohusu watu wengi
wanaozungumziwa (wao).
Wakati uliopo : ni wakati huu uliopo sasa. Kwa kitendo
kinachofanyika kila mara tunatumia wakati uliopo.
Mfano: Safi anakula viazi
Wao wanaenda shuleni
Wakati uliyopita: hutumika kuzungumzia vitendo ambavyo huwa vimetendwa nyakati zilizopita.
Mfano: Jana , nilienda sokoni
Juzi, mimi na baba tulikunywa chai ya maziwa
Wakati ujao: hutumika kuelezea vitendo ambavyo vitafanyika au kukamilika katika nyakati zijazo.
Mfano: Kesho, shangazi atakuja kunisalimia
Alhamisi, tutamaliza mkutano wetu
Share with your friends: |